Bnner

Breaking News
recent

WANAUME WENGI WANA TABIA YA KUCHEPUKA –DKT KIGWANGALLA



Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa wanaume wengi wamekuwa na tabia ya kuchepuka sana hivyo amewaasa wanaume kuacha tabia ya kuchepukaji kwenye ndoa ili waepuke kuwaambukiza wanawake Virusi vya Ukimwi (VVU).


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla

Dkt Kigwangalla ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Suzan Lyimo alietaka kujua
kwanini Wanawake wanakuwa idadi kubwa ya waathirika wa VVU, Je wewe waziri unatuambia nini kwanini wanawake wanakuwa na maambukizi kuliko wanaume Je, tatizo kuwa wanaume ndio wanaambukiza zaidi au wanawake wanakosa maadili?
“Wanawake wanaambukizwa zaidi kuliko wanaume kwasababu uwiano hauko mbali sana tofauti ni ndogo lakini kweli kwamba maumbile ya kibailojia ya wanawake ni tofauti sana na maumbile ya wanaume lakini pia lakini tabia za wanawake kuhusiana na ngono ni tofauti sana na tabia za wanaume kuhusiana na ngono wanaume wengi wana tabia ya kuchepuka sana na mara nyingi wanaweza waka vitoa virusi nje wakavileta kwenye ndoa zao kwa wanawake ambao wametulia hilo halibishaniwi,”alisema Kigwangalla.

“Kwahiyo nitoe rai kwa wanaume wenzangu kujipanga sana kwenye eneo hili la kuchepuka kuachana na michepuko lakini pia kupima afya zetu kupima hali zetu lakini pia kupima hali za wenza wetu kwa wale ndugu zangu waislam tumepewa fursa ya kuoa hadi  wanne, kwahiyo ni bora ukawa na wake nne kuliko kwenda kuwa na mtu usio mjua huko mtaani ni bora ukapima ukajiridhisha unaeenda kumuoa yuko salama na ukatulia na wake zako wanne.”


No comments:

Powered by Blogger.