T.I. APATA SHAVU KWENYE TAMTHILIA YA ‘ATLANATA MOST WANTED
T.I. ameongeza idadi ya wasanii wa muziki wanaoingia katika uigizaji. Rapper huyo amepata shavu la kuigiza kwenye tamthilia mpya ya ‘Atlanta’s Most Wanted’ itakayoonyeshwa kupitia kituo cha runinga cha Fox.
Katika tamthilia hiyo msanii huyo ameigiza kama Marcus Armstrong, mtoto wa mhalifu maarufu mjini Atlanta ambaye ni mmoja ya watu wakubwa wanaofanya kazi katika kundi linalojihusisha na biashara haramu.
“I am honored to partner with Fox and Bruckheimer on what is truly a passion project for me. It’s going to be amazing to see my city represented in this fashion,” T.I. ameiambia The Hollywood Reporter.
No comments: