Bnner

Breaking News
recent

TUNATAKA TUWE NA VIWANDA VINGI SIO HOTELI –RAIS MAGUFULI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema Tanzania inatakiwa kuwa na viwanda vingi na sio hoteli nyingi.


Rais Magufuli ameyasema hayo jana wakati akizindua rasmi maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.

“Basi tuangalie masuala ambayo ni very positive kwa taifa hili,tunataka tuwe na viwanda vingi sio hoteli nyingi. Tunataka watu watu wetu hata ukijenga hata kama ni kiwanda kimoja tu, hizo hela ulizoziplan zitatengeneza ajira za Watanzania, na serikali itapata revenue na kwa bahati nzuri sasa hivi Watanzania wameamka katika suala la ulipaji kodi”

Hata hivyo Rais Magufuli amewapongeza Watanzania kwa kuendelea kulipa kodi sambamba na kuwapongeza TRA kwa kuwaongeza siku wananchi za kuendelea kulipa kodi.

No comments:

Powered by Blogger.