TRUMP ATOA MASHARTI MAPYA YA USAFIRI KWA NCHI 6 ZA KIISLAM
Utawala wa rais Trump umeweka
masharti mapya ya maombi ya Visa kutoka kwa mataifa sita ya Kiislamu
pamoja na wakimbizi wote, ambayo yanawataka kuwa na mtu wanaohusiana ama
ushirikiano wa kibiashara na Marekani.
Masharti hayo mapya yalioanza kufanya kazi siku ya Alhamisi yanaelezea mahusiano ya kifamialia kama mzazi, mkeo ama mumeo,mtoto wa kiume ama wa kike.
Masharti hayo yanajiri baada ya mahakama kuu nchini Marekani kuidhinisha kwa muda agizo la rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa Waislamu.
No comments: