Bnner

Breaking News
recent

MAREKANI YACHUNGUZA SHAMBULIO KUBWA LA MTANDAO

Siku za hivi karibuni uvamizi wa mitandao umeshika kasi duniani Mamlaka nchini Marekani imesema inachunguza shambulio kubwa la kimtandao ambalo limekumba mifumo ya kompyuta duniani kote.

Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.

Mashirika mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, idara za serikali, makampuni makubwa, na kampuni za usafirishaji ni miongoni mwa zilizoathirika.



Serikali ya Ukraine iliweka aina hii ya uvamizi wa mtandao uliofanywa hivi karibuni

Watumiaji wameambiwa komputa zao zimenasa mpaka walipe kiasi cha dola mia tatu katika akaunti isiyofahamika.

Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imewashauri watu wasilipe fedha hizo.
Huku ikisema hakuna uhakika kwamba, mafaili yaliyofungwa yatafunguka baada ya malipo hayo kufanyika.

Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na linaendelea sehemu nyengine duniani.

 

No comments:

Powered by Blogger.