SERIKALI YAWEKA MIKAKATI MIPYA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amesema mikakati ya serikali kuhusu maambukizi mapya ya Virus Vya Ukimwi ni kuweka kinga na kutoa elimu ya Afya kwa umma.
Hayo yamebainishwa na Dkt Kigwangalla leo akiwa Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge alitaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kupunguza maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi katika jamii?
“Mikakati tuliyonayo juu ya maambukizi mapya ya virus vya Ukimwi ni mingi sana, mkakati wa kwanza ni kinga kuzuia watu wasipate virusi vya Ukimwi kwa kutoa elimu ya Afya kwa umma, mkakati wa pili ni tiba ambapo tunatumia kliniki zaidi ya 2000 za CTC ambazo zimetafakari nchi nzima kwaajili ya kutoa ART dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, na tukiamini kwamba watu ambao wanatumia dawa wanapungua kiasi ambapo wanaweza wakaambukiza kwahiyo hata ikitokea bahati mbaya umefanya ngono ambayo sio protected anaweza asimuambukize partner wake,” alisema Dkt Kigwangalla.
“Kwahiyo tuna mkakati wakuongeza idadi ya watu ambao tunawatibu kwamba kila atakae pima akabainika na virusi vya Ukimwi kuanzia oktoba mwaka jana atatibiwa hapohapo na kupewa dawa za kupunguza virusi vya Ukimwi na huu ni mkakati mpya wa kisasa ambapo baada ya kutoa kinga tunatoa tiba zaidi na hiyo itapelekea kupunguza maambukizi mapya kwa kiasi kikubwa.”
No comments: