UJENZI WA BWENI KUWAPA NAFUU WANAFUNZI TANGA
Wanafunzi wa Sekondari ya Kilale mjini Tanga sasa wataondokana na
adha ya kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani kwenda shuleni baada ya
wananchi wa kata ya Kilale kuamua kujenga bweni kwa nguvu zao ili
kuwakomboa vijana hao kielimu.
Diwani wa kata hiyo MWAGILO SALEHE ADAMU amesema lengo la ujenzi huo ni kuwakwamua wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kilale ambapo baadhi yao hushindwa kumaliza masomo kutokana na kutembea umbali mrefu kutokana na vikwazo wanavyokutana navyo njiani ukiwemo ujauzito.
Aidha walimu wa shule hiyo wamekiri kuwepo kwa changamoto nyinginezo kwa wanafunzi ikiwemo kukosa masomo kutokana na kutofika darasani kwa wakati hali inayoshusha kiwango cha ufaulu shuleni hapo.
Hata hivyo bweni hilo litakapokamilika litakuwa na jumla ya vyumba vyenye uwezo wa kulaza wanafunzi wa kike 200 huku juhudi za kujenga bweni la wanafunzi wa kiume zikiwa mbioni.

No comments: