BAJETI MWAKA 2017/2018 NANI WAMENUFAIKA, NANI HAWAJANUFAIKA
Hatimaye bajeti ya mwisho ya serikali ya Jubilee kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu Agosti 8, imesomwa huku wengi wakiitaja kuwa bajeti ya mwananchi kufuatia kuondolewa kwa ushuru mahindi yote yatakayoagizwa nchini kwa kipindi cha miezi minne. Akisoma bajeti hiyo ya 2017/2018 wa kifedha, Waziri wa Fedha Henry Rotich amesema hatua hiyo inalenga kumjali Mkenya wa kawaida.
Katika bajeti hiyo, watu wenye ulemavu, wakulima, wazee wenye umri zaidi ya 70, maafisa wa usalama vile vile ni miongoni mwa wanaotarajiwa kunufaika na bajeti hiyo ambayo imeangazia zaidi changamoto za wakenya na utimizaji wa miradi iliyosalia kabla ya uchaguzi mkuu kuandaliwa. Mwanzo waziri ametangaza kuondolewa kwa kodi zote zinazotozwa kwenye unga wa ugali na ngano kwa kuzingatia kuwa mkate na ugali ni miongoni mwa bidhaa zinazotumika nchini.
Kwenye bajeti hii aidha kiwango cha chini cha mshahara unaoweza kutozwa kodi kimeongezwa kutoka shilingi elfu kumi na moja mia moja thelathini na tano hadi elfu 13486 kumaanisha yeyote anayepokea chini ya kiwancho hicho hataozwa kodi aiana ya PAY.
Wazee wote wenye umri zaidi ya 70 watapokea kiwango fulani cha pesa kila mwezi na kulipiwa da za Bima ya Taifa NHIF na serikali. Pendekezo hilo vilevile litawanufaisha watu wenye ulamavu na yatima.
Kwa upande wao maafisa wa usalama ambao wengi wamekuwa wakilalamikia makazi sasa wameteNgewa shiligi bilioni moja nukta nne ambazo zitatumika kujenga majumba zaidi ya 1500. Vileviel vykba zaidi vitajengwa kwa ushirikiano na Benki ya AFDB. Shilingi bilioni 1.5 zitatumika kuendeleza mpango wa Bima ya Afya kwa maafisa hao.
Kwa upande wakulima wamelengwa kwenye mapendekezo yatakayowanufaisha likiwamo kutengwa kwa shilingi bilioni 4.1 kwa mbolea ya bei nafuu, shilingi bilioni moja kwa wakulima wa Miraa na shilingi 250 kuboresha huduma katika kiwandacha maziwa cha NEW KCC.
Kwenye hotuba ya leo, Waziri Rotich amependekeza kuondolewa kwa kodi inayotzwa magari ya kitalii yanayounganishwa nchini ili kuipiga jeki sekta hiyo. Kodi nyingine iliyoondolewa ni ya bidhaa zinazotumika katika viwanda vya dawa za mimea huku pendekezo hilo likilenga kupunguza bei ya dawa za mimea.
Miongoni mwa masuala mengine aliyoayapa kipaumbele ni kukuzwa kwa huduma za uwekezaji zinazotimiza matakwa ya dini ya kiislamu ili kuwavutia zaidi wawekezaji wa dini hiyo.
Mbali na hayo wanakandarasi wa kimataifa sasa watawekewa sharti la kuagiza aslimia 40 ya bidhaa wanazotumia kufanikisha kandarasi zao kutoka humu nchini.
Hata hivyo kama ilivyotarajiwa bajeti ya mwaka ya mwaka haitashilingiliwa na wote hasa waraibu wa michezo ya Bahati Nasibu baada ya Waziri Rotich kuongeza kiwango cha ushuru knachotozwa mapato ya michezo hiyo hadi asilimia 50.
Vilevile kodi inayotozwa pombe aina ya spirits imeongezwa kutoka shilingi 175 kwa lita hadi shilingi 200 kwa lita.
Ili kufanikisha bajeti ya mwaka huu serikali inatarajiwa kukopa shilingi bilioni 524 ili kutosheleza bajeti ya takriba shilingi trilion 2.287. Kwa fedha hizi, shilingi trilioni 1.3 zitatumika kwa matumizi ya kila siku shilingi bilioni 640 zikitengewa maenendeleo.
Miongoni mwa miradi iliyotengewa kiasi kikubwa cha fedha ni wa Reli ya Kisasa uliotengewa shiilingi bilioni 75.6 na ujenzi na ukarabati wa barabara shilingi bilioni 175.
Kadhalika kuanzia Julai mwaka huu, serikali itaanza mpango wa kusawazisha mishahara ya wafanyakazi wote wa umma huku awamu ya kwanza ikitarajiwa kugharimu shilingi bilioni 20.
Kumbuka hii ndio bajeti ya mwisho kabla ya kuandaliwa kwa uchguzi mkuu na Waziri hakuchelea fursa hiyo kumpongeza rais kwa fursa ya kulihudumia taifa hili kwenye wizara hiyo muhimu.
No comments: