Bnner

Breaking News
recent

MTOTO ALIYENUSURIKA SYRIA AONEKANA KWA MARA YA KWANZA

Mtoto, Omran Daqneesh aliyenusurika kwenye shambulio baya la mabomu ya angani nchini Syria Agosti  mwaka jana ameonekana kwa mara ya kwanza kwenye mahojiano ya kituo cha runinga cha Lebanese TV akiwa mwenye afya nzuri na sura yenye tabasamu.

Omran Daqneesh (5) ambae picha yake ilizua gumzo mitandao baada ya kuoneshwa akiwa kwenye gari la kubebea wagonjwa kama majeruhi aliyenusurika kwenye mashambulio ya anga yaliyotekelezwa na majeshi yamayomuunga mkono Rais wa Syria, Bashar al-Assad na kuuua zaidi ya watu 265.
Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha Runinga cha Lebanese TV, Baba mzazi wa mtoto huyo amesema ni furaha kumuona mwanae ana afya na kurudi katika hali yake ya kawaida kama zamani .

Baba mzazi wa Omran akiwa kwenye mahojiano na kituo cha runinga cha Lebanese Tv
Ulikuwa usiku wa jehanamu kwa wakazi wengi wa Allepo kwani giza na milio mizito ya mabomu ilisikika kila sehemu huku kukiwa na giza kali tukatoka na mke wangu huku tukiwa na watoto wawili pasikujua Omran yuko wapi? tulikata tamaa kwani nyumba yetu karibia yote ilikuwa imelipuliwa na mabomu ilikuwa kama ndoto siku mbili baadae tukaona picha zake kwenye magazeti, sikuamini,”amesema baba mzazi wa Omran.

Baba mzazi huyo wa Omran amesema kwa sasa mtoto wake anaendelea vizuri na anaonekana mwenye furaha tofauti na hali ilivyokuwa awali ingawaje bado anaogopa kila akisikia ndege zikipita angani.

Omran katikati akiwa na dada yake ambao wote walinusurika kwenye mashambulio ya mabomu mwaka jana.
Najisikia faraja ninapomuangalia mwanangu akiwa na tabasamu akicheza na wenzake japo muda mwingine akiona ndege angani hukimbilia ndani ila anaanza kuzoea sasa,“amesema mzazi wa Omran ambae hakutaka jina lake liwekwe wazi kwa kuhofia usalama wake.
Hata hivyo mzazi huyo amesema tangia mwaka jana amekuwa kimya kumuonesha mwanae kwenye vyombo vya habari akihofia kutekwa na kuchukua uamuzi wa kubadilisha jina la Omran baada ya jina na picha zake kusambaa dunia nzima huku akikiri kuwa alipewa ofa ya kuihama Syria lakini alikataa.
Mvulana Omran mwenye umri wa miaka minne
Picha ya Omran mpaka sasa inatumiwa kama nembo ya kuashilia maovu yaliyotendeka mjini Allepo nchini Syria yaliyotekelezwa na wanamgambo wa ISIS,Tazama picha za mtoto huyo akiwa kwenye muonekano wake wa sasa


No comments:

Powered by Blogger.