WATU WENYE SILAHA WASHAMBULIA ENEO LA WATALII MALI
Vyombo vya Usalama nchini Mali
vinasema vimeokoa zaidi ya wageni thelathini kutoka katika kituo kimoja
cha Utalii, kilichokuwa kikishambuliwa na watu waliokuwa na silaha.
Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Usalama, mmoja wa washambuliaji hao alifanikiwa kutoroka, baada ya kujeruhiwa, huku akiacha bunduki na chupa zilizokuwa na vifaa vya milipuko.
Majeshi ya Mali na Ufaransa yalifika katika eneo la tukio.
Kituo hicho cha utalii ni maarufu nyakati za juma la wiki na kuwa kivutio kwa raia wa Mali wenye uwezo na wale wa kigeni wanaoishi Bamako.
Mapema mwezi huu, Ubalozi wa Marekani mjini Bamako ulionya uwezekano wa kutokea mashambulizi katika siku za baadaye katika majengo ya wanadiplomasia wa magharibi na maeneo mengine katika mji wa Bamako ambako raia wa nchi za magharibi wanapenda kwenda.
No comments: