RAIS MAGUFULI AMEMWAMBIA MAMA ANNA MGHWIRA LEO IKULU
Baada ya kumuapisha Anna, President Magufuli amemtaka kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuondoa kero zinazowakabili Wananchi wa Kilimanjaro bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa, dini, makabilia na kanda wanazotoka.
Pia amemuhakikishia ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake na asikubali kuyumbishwa na mtu yeyote katika majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.
“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu, na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro, wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi” – Rais Magufuli.
Mama Anna Mghwira pia alipata nafasi ya kuzungumza na kumshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na amemuahidi kuwa yupo tayari kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kujenga Taifa.
“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo” – Anna Mghwira
No comments: