SIJUTII KUWA SEHEMU YA HIP HOP – MANSU-LI
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Mansu-Li amesema hajutii kuchagua kufanya aina hiyo ya muziki.
Rapper huyo anayefanya vizuri sasa na wimbo wake mpya ‘Hip Hop’, ameiambia EA Radio kuwa muziki wa hip hop aliupenda tangu akiwa shule ya msingi na hadi sasa anafurahia kuwa sehemu ya muziki huo.
“Sijawahi kujuta kwa sababu ya hip hop music au kuwa mwana hip hop, mimi nimekuwa shabiki wa hip hop tangu kipindi hicho hata sijui kama nitakuja kuwa mwanamuziki.
“Kwanza hadi sometime huwa najiuliza hivi kwa nini nilichagua hip hop, yaani nakosa jibu. Tangu nikiwa mdogo time hiyo nasikiliza ngoma za nje hata sijui wanachoongelea, ni vibe tu, nafurahia naona ni kitu fulani safi sana, kwa hiyo sijutii kuwa sehemu ya hip hop,” amesema Mansu-Li.
No comments: