JONAS MKUDE KULIPWA MAMILIONI SIMBA SC.
Baada ya vuta nikuvute ya Klabu ya Simba na Nahodha wao
Jonas Mkude kuhusu kuongeza mkataba sio siri tena kuwa mchezaji huyo
atasalia klabuni hapo na atakuwa ndiyo mchezaji anaepokea mkwanja mrefu
kuliko wote klabuni hapo kwa mwezi.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa
Mkude atalipwa kiasi cha Shilingi milioni 5 za kitanzania kwa mwezi nje
ya malupu lupu na posho ambazo watalipwa endapo timu yake itafanya
vizuri.
Mkude ambaye wiki hili kuliibuka Sintofahamu baada ya
tetesi kutoka kwa watu wake wa karibu wakidai kuwa huenda akaihama klabu
hiyo endapo hawatamuongezea mshahara amesaini mkataba wake mpya na
Simba SC jana na kuzima matumaini ya Klabu ya Yanga ambao walikuwa
wanawinda saini yake.
No comments: