HUU NI WAKATI WA KULINDA RASILIAMALI ZA NCHI – SPIKA NDUGAI
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema huu ni wakati wa kushirikiana na Serikali kuzilinda rasilimali za nchi ili watu wasizichezee kwa kuwa Taifa linahitaji maendeleo.
Spika wa Bunge,Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo
Tanzania(CCT), Askofu Dkt. Alex Malasusa
Spika Ndugai ametoa kauli Jumapili hii, katika harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania(CCT), katika tukio lililofanyika Mjini Dodoma, ambapo Spika Ndugai alikuwa mgeni rasmi na aliongoza Wabunge katika harambee hiyo.
“Kazi hiyo inatakiwa kufanywa na watu wote na hasa kwa wakati huu ambao rasilimali zimeanza kwenda ovyo bila ya kumnufaisha Mtanzania na kama zitaachwa kupotea bure hazitaonyesha thamani halisi kwa mtu wa chini,” alisema Ndugai.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Alex Malasusa amesema mpango wa ujenzi wa jengo hilo ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhamia Dodoma.
No comments: