HATA KAMA IKULU HAWAJALIPIA BILI YA MAJI KATA – RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameagiza taasisi zote hata ziwe za serikali zisipolipa bili za maji zikatwe maji hata kama ni Ikulu.
Rais ameyasema hayo jana akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambapo alizungumzia mradi wa maji na ulipaji katika taasisi zote.
“Mtu asipolipa bili, iwe taasisi yoyote hata kama ni Ikulu, narudia kusema kata.Kwa sababu tumezoa kudekezana, kwenye mawizara haya nafahamu, fedha za OC na hata fedha za bajeti wanazo, lakini suala la bili ya maji linakuwa si la lazima.”
No comments: